The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Traducer [Al-Humaza] - Swahili translation - Rowad Translation Center
Surah The Traducer [Al-Humaza] Ayah 9 Location Maccah Number 104
Ole wake kila anayewakejeli watu kwa ishara na maneno.
Aliyekusanya mali na kuihesabu.
Anadhani ya kuwa mali yake itambakisha milele!
Hasha! Atavurumishwa katika Hutwama.
Na ni nini kitakachokujulisha ni nini Hutwama?
Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa.
Ambao unapanda nyoyoni.
Hakika huo utafungwa sawasawa nao wako ndani yake.
Kwenye nguzo zilizonyooshwa.