عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Hud [Hud] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah Hud [Hud] Ayah 123 Location Maccah Number 11

Alif Laam Raa.[1] Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimefanywa kuwa sawasawa, kisha zikapambanuliwa kwa kina, kilichotoka kwa Mwenye Hekima, Mwenye habari zote.

Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usiniongeleshe kuwatetea wale waliodhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa."

Na akasema, "Pandeni humo kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."

Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ndiyo ya haki. Na Wewe ndiye hakimu bora zaidi ya wote wanaohukumu.

Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya umma miongoni mwa wale walio pamoja nawe. Na zitakuwapo umma tutakazozistarehesha, na kisha zitaguswa na adhabu chungu itokayo kwetu.

Sisi tunasema: 'Baadhi ya miungu yetu imekusibu kwa baa.' Akasema, "Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika.

Badala ya Yeye. Basi nyinyi nyote nipangieni njama, na kisha msinipe muhula!

Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni mtanabahi kuwa hakika kina 'Aadi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina 'Aadi, kaumu ya Hud.

Akasema: Enyi kaumu yangu! Mnaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, naye akawa amenipa rehema kutoka kwake, je, ni nani atakayeninusuru kutokana na Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamnizidishii isipokuwa kuhasirika tu.

Kama kwamba hawakuishi huko kwa ustawi. Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru Mola wao Mlezi. Hebu zingatieni! Thamud walipotelea mbali!

Hakika Ibrahim alikuwa mvumilivu sana, mwenye huzuni kubwa, na mwepesi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Na wajumbe wetu walipomjia Lut, yakamuwia mabaya kwa sababu yao na akaona dhiki kubwa kwa sababu yao. Akasema: Hii ni siku ngumu sana!

Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu sana, Mwenye upendo mkubwa.

Akasema: Enyi kaumu yangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuyazingira yote mnayoyatenda.

Siku hiyo itakapokuja, nafsi yoyote haitazungumza isipokuwa kwa idhini yake. Basi miongoni mwao kutakuwa na walio mashakani na wenye furaha.

Ama wale waliojitia mashakani, hao watakuwa Motoni, humo watavuta pumzi na kuitoa kwa ugumu mkubwa.

Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini kukazuka kuhitilafiana ndani yake. Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayowahangaisha.

Basi, nyooka kama ulivyoamrishwa, wewe na wale wanaotubia kwa Mwenyezi Mungu pamoja nawe, wala msivuke mipaka. Hakika Yeye anayaona yote myatendayo.

Isipokuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu. Na kwa hiyo ndiyo Mwenyezi Mungu amewaumba. Na lilitimia neno la Mola wako Mlezi kwamba hakika nitaijaza Jahannam kwa majini na watu kwa pamoja.