عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Joseph [Yusuf] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah Joseph [Yusuf] Ayah 111 Location Maccah Number 12

Pale waliposema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, ilhali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yuko katika upotovu wa dhahiri.

Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na ilhali sisi ni kundi lenye nguvu kabisa, basi bila ya shaka sisi tutakuwa tumehasirika.

Na ukaja msafara, kisha wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Hii ni bishara njema! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema hayo wanayoyatenda.

Na yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf akamtamani kinyume cha nafsi yake, na akafungafunga milango. Akamwambia: "Njoo!" Yusuf akasema: Audhubillahi (ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu)! Hakika Yeye ni bwana wangu, aliniweka maskani nzuri, na hakika madhalimu hawafaulu.

Yusuf akasema: Yeye ndiye aliyenitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliyekuwa katika jamaa za mwanamke akasema: Ikiwa shati lake limechanwa kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo.

Na ikiwa shati lake limechanwa kwa nyuma, basi mwanamke amesema uongo, naye Yusuf ni katika wakweli.

Basi yule bwana alipoona shati lake limechanwa kwa nyuma, akasema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu ni vikuu.

Nami sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni yenye kuamrisha mno mabaya, isipokuwa kile alichorehemu Mola wangu Mlezi. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu mno, Mwenye kurehemu sana.

Yusuf akasema: Nifanye msimamizi wa hazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi mzuri, mwenye elimu sana.

Wakasema: Sisi tutamrai baba yake amwachilie, na bila ya shaka tutafanya hilo.

Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na atakayenijia nalo, atapewa shehena nzima abebayo ngamia. Nami ni mdhamini juu ya hilo.

Wakasema: Malipo yake ni kwamba yule ambaye litapatikana katika shehena lake, basi huyo ndiye malipo yake. Hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu.

Wakasema: Akiwa ameiba huyu, basi hakika nduguye vile vile aliiba hapo zamani. Lakini Yusuf akaliweka hilo kisiri katika moyo wake wala hakulionyesha kwao. Akasema: Nyinyi ndio mko katika pahali paovu zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayosingizia.

Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipokuwa yule tuliyemkuta naye kitu chetu. Hakika, hapo tutakuwa ni wenye kudhulumu.

Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Huzuni wangu mkubwa juu ya Yusuf! Na macho yake yakawa meupe kutokana na huzuni, na akaizuia bila ya kuidhirisha.

Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu tu sikitiko langu na huzuni wangu. Na ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi.

Akasema: Leo hakuna lawama yoyote juu yenu. Mwenyezi Mungu atawasamehe, naye ni Mwenye kurehemu zaidi kuliko wote wanaorehemu.

Wakasema: Tallahi! Hakika wewe bado ungali katika upotovu wako wa zamani.

Akasema: Nitakujawaombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana.