عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The night journey [Al-Isra] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The night journey [Al-Isra] Ayah 111 Location Maccah Number 17

Na tulimpa Musa Kitabu na tukakifanya kuwa ni uongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawaambia) kwamba msimfanye yeyote asiyekuwa mimi kuwa mtegemewa wenu.

Na pindi tukitaka kuuteketeza mji, tunawaamrisha wale wana starehe na taanusi wake, lakini wao wakaendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli ikathibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa.

Subhanahu Wa Taa'la, (Ametakasika na Ametukuka mbali) kabisa na hayo wanayoyasema.

Akasema Mwenyezi Mungu: Nenda! Na atakayekufuata katika wao, basi hakika Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yenu, malipo yaliyo mengi.

Hapo basi bila ya shaka, tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo. Kisha usingepata yeyote wa kukunusuru kutokana nasi.

Na amka usiku kwa ajili ya kufanya ibada kwayo, ni ziada ya sunna hasa kwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi akakunyanyua cheo kinachosifika.

Na yule ambaye Mwenyezi Mungu anamuongoa, basi huyo ndiye aliyeongoka. Na yule ambaye anampotoa, basi hutawapatia walinzi wowote badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali ya kuwa wanakokotwa juu ya nyuso zao, huku ni vipofu, mabubu, na viziwi. Na makazi yao ni Jahannamu. Kila ukifanya kuzimika, tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.

Sema, "Lau kuwa nyinyi mnazimiliki hazina za rehema za Mola wangu Mlezi, basi hapana shaka mngelizuia kwa sababu ya kuhofu kuzitumia. Na mtu tangu hapo tabia yake ni mchoyo mno!

Musa akasema, "Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha isipokuwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa utaangamizwa."

Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha majini yeye na wale waliokuwa pamoja naye wote.

Na wanasema, 'Subhana Rabbina (Ametakasika Mola wetu Mlezi)! Hakika ahadi ya Mola wetu Mlezi lazima itimizwe!'"

Sema, "Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Ar-Rahman (Mwingi wa rehema), kwa jina lolote mnalomwita. Hakika, Yeye ana majina mazuri zaidi." Wala usiswali Swala yako kwa sauti kubwa sana, wala usiifiche kwa sauti ndogo sana, bali shika njia ya kati na kati ya hizo.

Na sema: Alhamdulillah (sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) ambaye hakujifanyia mwana yeyote, wala hana mshirika yeyote katika ufalme, wala hana mlinzi yeyote wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.