عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The cave [Al-Kahf] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The cave [Al-Kahf] Ayah 110 Location Maccah Number 18

Kwa hakika tumevifanya vilivyoko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao ndio wenye vitendo vizuri zaidi.

Na hakika Sisi tutavifanya vyote vilivyo juu ya ardhi kuwa kama nchi iliyopigwa na ukame.

Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili yale ndilo lilihesabu sawa zaidi urefu wa muda waliokaa.

Isipokuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unaposahau, na sema: huenda Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uwongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.

Sema: Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi muda waliokaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi. Kuona vyema kulikoje kwake na kusikia kuzuri kulikoje! Hawana mlinzi yeyote isipokuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake.

Na soma yale uliyofunuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hakuna yeyote awezaye kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio yoyote isipokuwa kwake.

Na sema: Hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akufuru. Hakika Sisi tumewaandalia madhalimu Moto ambao kuta zake zitawazingira. Na wakiomba msaada, watasaidiwa kwa kupewa maji yaliyo kama mafuta yaliyotibuka, yatakayowababua nyuso zao. Ni kinywaji kiovu mno kilichoje hicho, na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia palipoje hapo!

Wala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Kiyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya.

Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Wala simshirikishi Mola wangu Mlezi na yeyote.

Na lau kuwa ulipoingia kitaluni kwako, ungelisema: Mashaallah (alitakalo Mwenyezi Mungu huwa)! Hakuna nguvu yoyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo zaidi na watoto kuliko wewe.

Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi.

Na Mola wako Mlezi ni Msamehevu, Mwenye rehema. Lau angeliwachukulia kwa mujibu wa yale waliyoyachuma, bila ya shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo.

(Musa) akasema: "Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka." Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyojia.

Akasema: In shaa Allah (Mwenyezi Mungu akitaka), utanikuta mvumilivu, wala sitaasi amri yako yoyote.

(Yule mtu) Akasema, "Je, sikukwambia kwamba hakika wewe hutaweza kusubiri kuwa pamoja nami?"

(Musa) Akasema, "Nikikuuliza kuhusu kitu chochote baada ya haya, basi usifuatane nami. Kwani hakika umekwishapata udhuru kutoka kwangu."

Basi tulitaka Mola wao Mlezi awabadilishie aliye bora zaidi kuliko huyo kwa kutakasika, na aliye karibu zaidi kwa huruma.

Akasema: Yale ambayo Mola wangu Mlezi ameniimarisha ndani yake ndiyo bora zaidi. Lakini nisaidieni kwa nguvu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi imara.

Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipoijaza sawasawa nafasi iliyo katikati ya milima miwili hiyo, akasema, "Pulizeni moto" mpaka alipokifanya kuwa moto, akasema, "Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimimine juu ya chuma hicho."

Akasema, "Hii ni rehema kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Na itakapokuja ahadi ya Mola wangu Mlezi, atakivunjavunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni ya kweli."

Sema: Lau kuwa bahari ingekuwa ndiyo wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingelimalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeliileta mfano wa hiyo kuongezea.