عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Prophets [Al-Anbiya] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Prophets [Al-Anbiya] Ayah 112 Location Maccah Number 21

Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kujua vyema.

Lau wangelikuwamo humo miungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingelihaliribika. Subahanallah (Ametakasika Mwenyezi Mungu), Bwana Kiti cha Enzi mbali na hayo wanayoyazua.

Yeye haulizwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaoulizwa kwa wayatendayo.

Na walisema: Arrahman (Mwingi wa rehema) alijifanyia mwana! Subhanahu (Ametakasika mbali na hayo!) Bali hao (wanaowaita wana) ni waja waliotukuzwa.

Na wanapoguswa na mpulizo mmoja tu wa adhabu itokayo kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka wao husema: Ole wetu! Hakika tulikuwa wenye kudhulumu.

Na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya mkishageuka kwenda zenu.

Na Ayyubu, alipomwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.

Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhabika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hakuna mungu isipokuwa Wewe Subhanaka (Uliyetakasika). Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.