عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Pilgrimage [Al-Hajj] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Pilgrimage [Al-Hajj] Ayah 78 Location Maccah Number 22

Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka juu ya kufufuliwa, basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu iliyogandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisichokuwa na umbo, ili tuwabainishie. Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunachokitaka mpaka muda uliowekwa. Kisha tunawatoa kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanaokufa, na wapo katika nyinyi wanaorudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapoyateremsha maji juu yake, husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri.

Hayo ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki, na kwamba hakika Yeye ndiye mwenye kuhuisha wafu, na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Na kwamba hakika Saa (ya Kiyama) itakuja hakuna shaka kwa hilo, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.

(Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya iliyoitanguliza mikono yako. Na hakika Mwenyezi Mungu si dhalimu kwa waja.

Humuomba yule ambaye bila ya shaka madhara yake yapo karibu zaidi kuliko manufaa yake. Kwa hakika huyo ni mlinzi muovu, na rafiki muovu.

Na namna hivyo tumeiteremsha (Qur-ani) kuwa ni Aya zilizo wazi, na hakika Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye.

Kwa maji hayo, vitayeyushwa vilivyomo matumboni mwao, na ngozi zao pia.

Na kwa ajili yao yatakuwapo marungu ya chuma.

Na pale tulipomweka Ibrahim pahala penye ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu, na wanaokaa hapo kwa ibada, na wanaorukuu, na wanaosujudu.

Ndiyo hivyo! Na anayetukuza alama za dini za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.

Na kila umma tumewafanyia mahali pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyoruzukiwa katika wanyama wa mifugo. Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Kwa hivyo, jisalimishieni kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu.

Na ngamia (na ng'ombe) wa zawadi ya Nyumba Tukufu, tumewafanyia kuwa ni kudhihirisha alama za dini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hao mna heri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanaposimama kwa safu. Na waangukapo kwenye ubavu, kuleni katika hao na walisheni waliokinai na wanaolazimika kuomba. Ndiyo kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru.

Wale ambao walitolewa majumbani mwao pasina haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingelivunjwa nyumba za watawa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayemsaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mtukufu.

Na wanakuharakisha ulete adhabu, lakini kamwe Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na ahadi yake. Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyohesabu nyinyi.

BIla ya shaka atawaingiza mahali watakapoparidhia. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi, Mstahamilivu.

Ndiyo namna hivi. Na anayelipiza mfano wa alivyoadhibiwa, kisha akadhulumiwa, basi hakuna shaka Mwenyezi Mungu atamsaidia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye maghfira.

Hawakumpa taadhima Mwenyezi Mungu anavyostahiki kupewa taadhima. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye nguvu, Mtukufu.

Mwenyezi Mungu huteua Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.