عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Believers [Al-Mumenoon] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Believers [Al-Mumenoon] Ayah 118 Location Maccah Number 23

Kisha tukamfanya kuwa tone la mbegu ya uzazi katika mahali patulivu palipo madhubuti.

Kisha tukaliumba tone hilo kuwa damu iliyoganda, na tukaiumba damu hiyo kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande hilo la nyama kuwa mifupa, na mifupa hiyo tukaivisha nyama. Kisha tukamfanya kuwa kiumbe mwingine. Basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa baraka, Mbora zaidi wa waumbaji.

Akasema (Nuhu), "Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha."

Basi utakapotulia sawasawa wewe na wale walio pamoja nawe humo merikebuni, sema: Alhamdulillahi (Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu), aliyetuokoa kutoka kwa kaumu madhalimu!

Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ndiye Mbora wa wateremshaji.

Akasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha.

(Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta.

Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipoinuka penye utulivu na chemchemi za maji.

Hata tutakapowatia katika adhabu wale waliodekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watakapoyayatika.

Na huku mkiitakabari na usiku mkiizungumzia (Qur-ani) kwa dharau.

Na lau tungeliwarehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo, bila ya shaka wangeliendelea katika upotofu wao, vile vile wakitangatanga.

Watasema, "Ufalme huo ni wa Mwenyezi Mungu." Sema: Basi vipi mnadanganyika?

Na sema: Mola wangu Mlezi! Ninajikinga kwako kutokana na wasiwasi wa mashetani.

Na ninajikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.

Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tukirudia tena (ya zamani), basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.