عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Standard [Al-Furqan] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Standard [Al-Furqan] Ayah 77 Location Maccah Number 25

Siku watakapowaona Malaika, hakutakuwa na furaha yoyote siku hiyo kwa wahalifu. Na watasema, "Mwenyezi Mungu apishe mbali!" Na tutayajia yale waliyoyatenda katika vitendo vyao, na tuvifanye kuwa mavumbi yaliyotawanyika.

Wala hawatakuletea mfano wowote, isipokuwa na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora zaidi.

Na wanapoambiwa: Msujudieni Arrahman (Mwingi wa rehema!) Wao husema: Ni nani Arrahman (Mwingi wa rehema)? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe tu? Na huwazidishia kujitenga mbali.