عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Poets [Ash-Shuara] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Poets [Ash-Shuara] Ayah 227 Location Maccah Number 26

Tw'a Siin Miim.[1]

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Akasema: Mola wangu Mlezi, hakika mimi ninachelea kwamba watanikadhibisha.

Na wao wana dhambi niliyowafanyia, kwa hivyo ninahofu wanaweza kuniua.

Akasema: Sivyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza.

Basi nendeni kwa Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

(Firauni) akasema: Je, sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa miongoni mwetu katika umri wako miaka mingi?

(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipokuwa miongoni mwa wale waliopotea.

Firauni akasema: Na ni nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote?

(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza.

(Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na vilivyo baina yake, ikiwa nyinyi mnatia akilini.

Akasema: Je, hata kama nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?

(Firauni) akawaambia waheshimiwa waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu.

(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa!

Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Kwani hakika hao ni adui zangu, isipokuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Ambaye ndiye aliyeniumba, na Yeye ndiye ananiongoa

Tulipowafanya nyinyi ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwingi wa kurehemu.

Mimi si chochote isipokuwa ni Mwonyaji wa dhahiri shahiri.

Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikadhibisha.

Kwa hivyo tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye katika marikebu iliyosheheni.

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Haya si chochote isipokuwa ni mtindo wa watu wa tokea zamani.

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu.

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu.

Akasema: Hakika mimi ni katika wanaokichukia hiki kitendo chenu.

Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo.

Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale.

Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.

Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua zaidi.