عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

THE ANT [An-Naml] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah THE ANT [An-Naml] Ayah 93 Location Maccah Number 27

Na hakika wewe unafundishwa Qur-ani inayotokana kwake Mwenye hekima, Mwenye kujua zaidi.

Basi alipoufikia, ilinadiwa: Amebarikiwa aliyemo katika moto huu na walioko pembezoni mwake. Na ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Lakini aliyedhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya, basi Mimi hakika ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilogundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea habari za yakini.

Akasema (Suleiman): Tutatazama iwapo umesema ukweli au wewe ni miongoni mwa waongo.

Kwa hakika, imetoka kwa Suleiman nayo hakika ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.

Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri.

Basi alipofika (mjumbe) kwa Suleiman, alisema (Suleiman): Hivyo ndivyo nyinyi mnanisaidia kwa mali? Aliyonipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyowapa nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu.

Basi (Malkia) alipofika akaambiwa: Je, kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hiki. (Suleiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa elimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu.

Na yale aliyokuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yalimzuilia. Hakika yeye (Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri.

Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipoliona, alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Suleiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lililofanyiwa sakafu ya vioo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimejidhulumu, na sasa ninanyenyekea pamoja na Suleiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu; lakini nyinyi ni watu mnaojaribiwa.

Sema: Alhamdu Lillahi (Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu!) Na amani ishuke juu ya waja wake aliowateua. Je, Mwenyezi Mungu ndiye bora, au wale wanaowashirikisha naye?

Na Siku tutakapokusanya kutoka katika kila umma kundi miongoni mwa wale wanaokadhibisha Ishara zetu, nao watagawanywa mafungu mafungu.

Na sema, "Alhamdu Lillahi (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu). Yeye atawaonyesha Ishara zake, na mtazijua. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika mbali na hayo myatendayo.