عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Spider [Al-Ankaboot] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Spider [Al-Ankaboot] Ayah 69 Location Maccah Number 29

Alif Lam Mim.[1]

Mwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu, basi hakika miadi ya Mwenyezi Mungu itafika bila ya shaka. Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua zaidi.

Na anayefanya juhudi, basi bila ya shaka anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu.

Na katika watu yupo yule anayesema, "Tumemuamini Mwenyezi Mungu." Lakini anapopewa maudhi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, anayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapokuja nusura kutoka kwa Mola wako Mlezi, kwa yakini husema, "Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi." Kwani Mwenyezi Mungu hayajui zaidi yaliyomo vifuani mwa walimwengu?

Akasema, "Ewe Mola wangu Mlezi, ninusuru kutokana na watu waharibifu hawa!"

Lakini walimkadhibisha, basi ukawatwaa mtikiso wa ardhi, wakapambazukiwa ndani ya nyumba zao nao wameanguka kifudifudi.

Kwa hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu wanachokiomba badala yake Yeye. Na Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Na walisema, "Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Sema, "Hakika Ishara ziko tu kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu."

Na ni wanyama wangapi hawawezi kujimilikia riziki zao! Mwenyezi Mungu anawaruzuku hao na nyinyi pia. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua zaidi.

Na ukiwauliza: Ni nani anayeteremsha maji kutoka mbinguni, na akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake? Bila ya shaka watasema: Ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdu Lillahi (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu). Bali wengi katika wao hawatumii akili.

Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi hakika tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema.