عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Coalition [Al-Ahzab] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Coalition [Al-Ahzab] Ayah 73 Location Maccah Number 33

Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.

Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayesema kweli, naye ndiye anayeongoa Njia.

Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wanaume watiifu na wanawake watiifu, na wanaume wakweli na wanawake wakweli, na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri, na wanaume wanyenyekevu na wanawake wanyenyekevu, na wanaume watoao sadaka na wanawake watoao sadaka, na wanaume wanaofunga saumu na wanawake wanaofunga saumu, na wanaume wanaojihifadhi tupu zao, na wanawake wanaojihifadhi tupu zao, na wanaume wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi na wanawake wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.

Hao wa zamani, waliokuwa wakifikisha jumbe za Mwenyezi Mungu na wanamwogopa Yeye, na wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu.

Ewe Nabii, tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao, na uliowamiliki kwa mkono wako wa kulia katika wale aliokupa Mwenyezi Mungu, na mabinti wa ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama yako waliohama pamoja nawe; na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwa Nabii, kama mwenyewe Nabii akitaka kumuoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Sisi tunajua tuliyowafaradhishia wao katika wake zao na wanawake iliyowamiliki mikono yao ya kulia, ili isiwe dhiki kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Enyi mlioamini, msiingie katika nyumba za Nabii isipokuwa mpewe ruhusa kwenda kula chakula, siyo kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni, na mkishakula, tawanyikeni, wala msiweke hapo mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii, naye anawastahi, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki. Na mnapowauliza wakeze haja, waulizeni kwa nyuma ya mapazia. Hivyo ndivyo usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haikufailiini kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu.

Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri na amewaandalia Moto unaowaka kwa nguvu.