عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Saba [Saba] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah Saba [Saba] Ayah 54 Location Maccah Number 34

Na walisema wale waliokufuru: "Haitatufikia Saa ya Kiyama." Sema: Kwani hapana shaka itakufikieni, ninaapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi, isipokuwa vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha.

Tukamwambia: "Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayoyatenda."

Naye Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyeyushia chemichemi ya shaba. Na katika majini, walikuwako waliokuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamuonjesha adhabu ya Moto unaowaka.

Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na vitu vifananavyo vingine, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yaliyo madhubuti. Enyi watu wa Daudi, fanyeni kazi kwa kushukuru. Na ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.

Lakini wakasema, "Mola wetu Mlezi! Weka mwendo mrefu baina ya safari zetu." Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi tu, na tukawatawanya tawanya. Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru mno.

Na hatukumtuma mwonyaji yeyote kwenye mji, isipokuwa walisema wale waliojidekeza kwa starehe zao, wa mji huo, "Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo."

Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyowapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!

Sema: "Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema ya ghaibu."

Sema: "Ikiwa mimi nimepotea, basi nimepotea kwa kudhuru nafsi yangu mwenyewe. Na ikiwa nimeongoka, basi ni kwa sababu ya kunifunulia Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, aliye karibu."