عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Those who set the ranks [As-Saaffat] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah Those who set the ranks [As-Saaffat] Ayah 182 Location Maccah Number 37

Ninaapa kwa wanaojipanga kwa safu.

Hakika mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.

Bali unastaajabu, na wao wanafanya masihara.

Na husema: Haya si chochote isipokuwa ni uchawi tu ulio dhahiri.

Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.

Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.

Wako juu ya viti mfano wa kitanda wameelekeana.

Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha, mazuri.

Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nilikuwa na rafiki.

Atasema: Wallahi! (Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu) Ulikaribia sana kunipoteza.

Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa waliohudhurishwa.

Mashada ya matunda yake kama kwamba ni vichwa vya mashetani.

Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu.

Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani.

Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?

Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyovichonga wenyewe?

Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekuumbeni nyinyi na hivyo mnavyovifanya!

Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.

Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.

Basi alipofika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Insha Allah (Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri.

Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.

Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu waliokuja baadaye.

Na tukawaachia (sifa njema) katika watu waliokuja baadaye.

Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.

Isipokuwa mwanamke mkongwe katika wale waliobakia nyuma.

Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walioshindwa.

Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?

Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!

Ametakasika Mwenyezi Mungu mbali na hayo wanayomsingizia.

Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.

Bila ya shaka tungelikuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumkusudia Yeye tu.

Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakaonusuriwa.

Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.