عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Troops [Az-Zumar] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Troops [Az-Zumar] Ayah 75 Location Maccah Number 39

Uteremsho wa Kitabu hiki umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Sema: Mwenyezi Mungu tu namuabudu kwa kumsafishia Yeye tu Dini yangu.

Je, yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi (ni sawa na mwenye moyo mgumu?) Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisizomkumbuka Mwenyezi Mungu! Hao wamo katika upotofu wa dhahiri.

Je, atakayekuwa anapambana kwa uso wake na adhabu mbaya kabisa Siku ya Kiyama, (ni sawa na watenda wema?) Na wataambiwa wenye kudhulumu: Onjeni hayo mliyokuwa mkiyachuma!

Na ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi hana wa kumpotoa. Je, Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu, anayeweza kulipiza?

Isije ikasema nafsi: Ee majuto yangu kwa yale niliyopoteza upande wa Mwenyezi Mungu, na hakika nilikuwa miongoni mwa wanaofanya maskhara!

Au ikasema: Ingelikuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye kumcha Mungu.

Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa waliokuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu matendo yako yataharibika, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kuhasiri.

Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.

Na utawaona Malaika wakizunguka pembeni mwa Kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, wakimtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi. Na patahukumiwa baina yao kwa haki na patasemwa: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote!