عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The wind-curved sandhills [Al-Ahqaf] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The wind-curved sandhills [Al-Ahqaf] Ayah 35 Location Maccah Number 46

Ha, Mim.[1]

Uteremsho wa Kitabu uliotoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Na kabla yake kilikuwapo Kitabu cha Musa, kuwa chenye uwongozi na rehema. Na hiki ni Kitabu cha kusadikisha na kilichokuja kwa lugha ya Kiarabu, ili kiwaonye wale waliodhulumu, na kiwe ni bishara njema kwa watendao mema.

Na yule aliyewafyonya wazazi wake: 'Uff kwenu nyote. Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa, na hali vizazi vingi vimekwisha pita kabla yangu!' Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu (na humwambia mtoto wao): 'Ole wako! Amini! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli.' Na yeye husema: 'Hayakuwa haya ila ni visa vya watu wa kale.'

Na wote watakuwa na daraja zao mbalimbali kwa waliyoyatenda, na ili awalipe kwa ukamilifu kwa vitendo vyao, na wala hawatadhulumiwa.