عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The victory [Al-Fath] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The victory [Al-Fath] Ayah 29 Location Madanah Number 48

Bila ya shaka wale wanaokupa kiapo cha utii, kwa hakika wanampa Mwenyezi Mungu kiapo cha utii. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Kwa hivyo, avunjaye ahadi hizi, basi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake. Na anayetekeleza aliyomuahadi Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.

Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wale walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kutokana na athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.