عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Table Spread [Al-Maeda] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Table Spread [Al-Maeda] Ayah 120 Location Madanah Number 5

Enyi mlioamini! Msivunje alama za Dini, za Mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu, wala wanyama wanaopelekwa Makka kuchinjwa kama zawadi, wala wale wanaotiwa vigwe, wala wale wanaoelekea kuiendea Nyumba Takatifu, wakitafuta fadhila kutoka kwa Mola wao Mlezi na radhi. Na mkishatoka katika Ihram, basi windeni. Wala kuwachukia watu kwa kuwa waliwazuia kuufikia Msikiti mtakatifu kusiwapelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na kupita mipaka. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kile kilichochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na yule aliyekufa kwa kunyongeka koo. Na yule aliyekufa kwa kupigwa, na yule aliyekufa kwa kuanguka, na yule aliyekufa kwa kupigwa pembe, na yule aliyeliwa na mnyama, isipokuwa mkimdiriki kumchinja, na yule aliyechinjiwa masanamu, na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni kupita mipaka. Leo wale waliokufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimewakamilishia Dini yenu, na nimewatimizia neema yangu, na nimeridhia Uislamu uwe ndiyo Dini yenu. Na mwenye kulazimishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Sala, basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake katika vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba, basi jisafisheni. Na mkiwa wagonjwa au katika safari, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi likusudieni vumbi lililo nzuri, na pakeni nyuso zenu na mikono yenu katika hilo. Hapendi Mwenyezi Mungu kuwatia katika uzito, bali anataka kuwatakasa na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.

(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi hakika nchi hiyo wameharamishiwa, kwa muda wa miaka arobaini watakuwa wakitangatanga katika ardhi. Basi wewe usiwasikitikie watu wavukao mipaka.

Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, yakiwa ni malipo ya waliyoyachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Lakini mwenye kutubia baada ya dhuluma yake, na akatengenea, basi Mwenyezi Mungu ataipokea toba yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru, miongoni mwa wale waliosema kwa vinywa vyao, "Tumeamini", na hali nyoyo zao hazikuamini, na miongoni mwa Mayahudi, wanaosikiliza sana uongo, wanaowasikiliza sana kaumu wengine ambao hawajakujia. Wao huyabadilisha maneno baada ya kuwekwa pahali pake. Wanasema, "Mkipewa haya, basi yachukueni, na msipopewa haya, tahadharini." Na yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumfitini, basi huwezi kuwa na uwezo kwa ajili yake mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu hataki kuzisafisha nyoyo zao. Wana hizaya katika dunia, na Akhera wana adhabu kubwa.

Na mwenye kumfanya rafiki wandani Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndio wenye kushinda.

Na wakadhani kuwa hapatakuwa majaribio; basi wakawa vipofu na viziwi. Kisha Mwenyezi Mungu akawapokelea toba zao. Kisha tena wengi katika wao wakawa vipofu na viziwi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona vyema hayo wayatendayo.

Hakika, wamekufuru wale waliosema: 'Hakika, Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryam!' Na hali Masihi mwenyewe alisema: 'Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia Bustani ya mbinguni, na pahali pake ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wowote wa kuwanusuru.

Je, hawatubii kwa Mwenyezi Mungu na wakamwomba awafutie dhambi? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Sema: Je, mnawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, wale ambao hawawamilikii kudhuru wala kunufaisha? Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Enyi mlioamini! Msiwaue mawindo hali ya kuwa mko katika Ihram (ya Hija au 'Umra). Na miongoni mwenu atakayemuua makusudi, basi malipo yake yatakuwa ni kuchinja kilicho sawa na alichokiua, katika mifugo, kama wanavyohukumu hivyo waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama huyo apelekwe kwenye Al-Kaaba, au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili. Mwenyezi Mungu amekwishayafuta yaliyopita. Lakini atakayefanya tena, Mwenyezi Mungu atamwadhibu vikali. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kuadhibu vikali.

Mwenyezi Mungu ameifanya Al-Kaaba, hii Nyumba Tukufu, kuwa ya kuwakimu watu, na Miezi Mitakatifu, na dhabihu walioletwa Makka kama zawadi, na dhabihu waliofungwa vigwe. Hayo ni ili mjue ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika mbingu na yaliyo katika ardhi, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.

Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Hakuna kilicho juu ya Mtume isipokuwa kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnachokidhihirisha na mnachokificha.

Na pale Mwenyezi Mungu aliposema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipokutia nguvu kwa Roho Mtakatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utu uzimani. Na nilivyokufunza kuandika na hekima na Taurati na Injili. Na ulipokuwa unatengeneza kutoka katika udongo kama umbo la ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ndani yake na likawa ndege kwa idhini yangu; na ulipowaponya vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipowafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipokukinga na Wana wa Israili ulipowajia na hoja zilizo wazi, na wakasema wale waliokufuru miongoni mwao: Haya si lolote isipokuwa uchawi ulio wazi!

Akasema Isa bin Maryam: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshie meza yenye chakula kutoka mbinguni ili kiwe kwetu Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora zaidi wa wanaoruzuku.

Na pale Mwenyezi Mungu aliposema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, wewe ndiye uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu wawili badala ya Mwenyezi Mungu? (Isa) akasema: Subhanaka (Wewe umetakasika)! Hainifailii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema, basi bila ya shaka umekwishayajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mwenye kujua vyema yale yaliyofichikana.