عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The winnowing winds [Adh-Dhariyat] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The winnowing winds [Adh-Dhariyat] Ayah 60 Location Maccah Number 51

Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka ni kweli.

Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.

Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayohitalifiana.

Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.

Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani ya mbinguni na chemchemi.

Kwa hivyo, akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: 'Usiwe na hofu.' Basi wakambashiria kupata kijana mwenye elimu.

Ndipo mkewe akawaelekea kwa sauti ya kelele huku anajipiga usoni kwa mastaajabu, akasema: "Mimi ni kikongwe na tasa!"

Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyosema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua.

Yaliyotiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanaopindukia mipaka.

Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: 'Huyu ni mchawi au mwendawazimu!'

Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio wenye uwezo wa kuzitanua.

Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.

Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.