عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The moon [Al-Qamar] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The moon [Al-Qamar] Ayah 55 Location Maccah Number 54

Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: 'Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!'

Ikawa inakwenda kwa macho yetu, kuwa ni malipo kwa alivyokuwa amekanushwa.

Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anayekumbuka?

Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anayekumbuka?

Kina 'Adi walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?

Ni yeye tu aliyeteremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mno mwenye mshari mkubwa!

Na waambie kwamba hakika maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliyehusika.

Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?

Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo.