عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Event, The Inevitable [Al-Waqia] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Event, The Inevitable [Al-Waqia] Ayah 96 Location Maccah Number 56

Hao ndio watakaowekwa karibu (na Mwenyezi Mungu).

Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyotonewa.

Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchemi safi.

Wanapendana na waume zao, hirimu moja.

Katika upepo wa moto, na maji yanayochemka.

Tena mtakunywa kama wanavyokunywa ngamia wenye kiu.

Hiyo ndiyo karamu yao ya kuwakaribisha Siku ya Malipo.

Je, mnaiona mbegu ya uzazi mnayoidondokesha?

Mkisema: 'Hakika sisi tumegharimika.'

Na hakika bila ya shaka hiki ni kiapo kikubwa, laiti mngelijua!

Hakika hii bila ya shaka ni Qur-ani Tukufu.

Ni uteremsho unaotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?

Kwa nini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?

Kwa hivyo, akiwa miongoni mwa wale walio karibu na Mwenyezi Mungu.

Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa wale wa upande wa kulia.

Basi karamu ya makaribisho yake ni maji yanayochemka.