عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Iron [Al-Hadid] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Iron [Al-Hadid] Ayah 29 Location Madanah Number 57

Kinamsabihi kumtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo ndani ya mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Watawaita wawaambie: 'Kwani hatukuwa pamoja nanyi?' Watawaambia: 'Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkatazamia mabaya (Waumini), na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni mpaka ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu yule[1] akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.

Kwa hakika wanaume wanaotoa sadaka, na wanawake wanaotoa sadaka, na wakamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, watazidishiwa maradufu na watapata malipo ya ukarimu.