عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Exile [Al-Hashr] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah Exile [Al-Hashr] Ayah 24 Location Madanah Number 59

Vinamtakasa Mwenyezi Mungu vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyofichikana na yanayoonekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anayefanya analolitaka, Mkubwa. Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayomshirikisha nayo.