عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Mutual Disillusion [At-Taghabun] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah Mutual Disillusion [At-Taghabun] Ayah 18 Location Madanah Number 64

Yeye ndiye aliyekuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mno mnayoyatenda.

Hayo ni kwa kuwa Mitume wao walikuwa wakiwajia kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: 'Hivyo binadamu ndio atuongoe?' Basi wakakufuru, na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, si mhitaji, naye ni Msifiwa.

Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni maradufu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukrani, Mstahamilivu.