عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Sovereignty [Al-Mulk] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The Sovereignty [Al-Mulk] Ayah 30 Location Maccah Number 67

Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uwezo mno juu ya kila kitu.

Na kwa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo!

Na watasema: 'Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa tukitumia akili, tusingelikuwa katika watu wa Moto wenye mwako mkali!'

Au mnadhani mko salama kutokana na aliyeko juu ya kuwa Yeye hatakupelekeeni kimbunga chenye changarawe? Basi mtajua vipi maonyo yangu?

Na bila ya shaka walikwisha kanusha wale waliokuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu?

Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanakakamia tu katika jeuri na kujiweka mbali.

Sema: Hakika elimu ya hayo iko kwa Mwenyezi Mungu; na hakika mimi ni mwonyaji wa wazi tu mwenye kubainisha.