عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The heights [Al-Araf] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The heights [Al-Araf] Ayah 206 Location Maccah Number 7

Alif Laam Miim Swaad.[1]

Kitabu kilichoteremshwa kwako, basi isiwe dhiki yoyote katika kifua chako kwa sababu yake, ili uonye kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini.

(Mwenyezi Mungu) akasema, "Ni nini kilichokuzuia kusujudu nilipokuamrisha?" Akasema, "Mimi ni bora zaidi kumliko yeye. Uliniumba kwa moto, naye ulimuumba kwa udongo."

Akasema, "Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula."

Na baina yao (makundi mawili hayo) patakuwapo pazia. Na juu ya Minyanyuko patakuwa watu watakaomjua kila mmoja kwa alama zao, na wao watawaita watu wa Peponi: Salamu Alaykum (amani iwe juu yenu)! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai.

Na ardhi nzuri mimea hutoka yake kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Nayo ardhi ambayo ni mbaya haitoki isipokuwa mimea michache, isiyokuwa na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara (Aya) kwa kaumu wanaoshukuru.

Wale watukufu katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika upotofu ulio dhahiri.

Akasema: Enyi watu wangu! Mimi siko katika upotofu, lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.

Akasema: Enyi watu wangu! Mimi sina upumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.

Nawafikishia ujumbe wa Mola wangu Mlezi. Na mimi kwenu ni mwenye kuwanasihi, mwaminifu

Basi tetemeko la ardhi likawanyakua, na kulipokucha wakawa majumbani mwao kifudifudi wamekwishakufa.

Basi tetemeko la ardhi likawachukua, kwa hivyo wakawa katika makazi yao wameanguka kifudifudi.

Je, wana amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawawi na amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu waliohasiri.

Wala hatukuwapata wengi wao wakiwa ni wenye kushika agano lolote, bali kwa hakika tuliwapata wengi wao ni wavukao mno mipaka.

Inastahiki zaidi juu yangu kwamba nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu. Hakika nimewajia na Ishara za waziwazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi waachilie pamoja nami Wana wa Israili."

Akasema: Ndiyo! Nanyi bila ya shaka ni katika waliotiwa karibu nami.

Akasema, "Je, niwatafutie mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye aliyewaboresha kuliko walimwengu wote?"

Na wakati mambo yalipoangushwa katika mikono yao, na wakaona ya kwamba wamekwishapotea, wakasema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hataturehemu na akatufutia dhambi, basi bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa waliohasiri.

(Musa) akasema: Mola wangu Mlezi! Nifutie dhambi mimi na kaka yangu, na utuingize katika rehema yako. Nawe ni Mwenye kurehemu zaidi kuliko wote wenye kurehemu.

Na pale alipotangaza Mola wako Mlezi kwamba hakuna shaka atawaletea watu ambao watawaadhibu kwa adhabu mbaya mpaka Siku ya Kiyama. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na Mwenye kurehemu.

Na kama uchochezi kutoka kwa Shetani utakuchochea, basi tafuta ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Msikizi mzuri, Mwenye kujua vyema.