عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The man [Al-Insan] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah The man [Al-Insan] Ayah 31 Location Madanah Number 76

Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.

Na atawajazi Bustani za mbinguni na maguo ya hariri kwa vile walivyosubiri.

Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya atilasi. Na watavishwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.

Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.