عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Spoils of war, booty [Al-Anfal] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah Spoils of war, booty [Al-Anfal] Ayah 75 Location Madanah Number 8

Mlipokuwa mnamuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akawaitikia kuwa Mimi hakika nitawasaidia kwa elfu moja miongoni mwa Malaika wakifuatana mfululizo.

Na Mwenyezi Mungu hakufanya hayo isipokuwa yawe ni bishara na ili nyoyo zenu zitue kwayo. Na nusura haiwi isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Kwa hivyo, hamkuwaua nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua. Nawe hukutupa ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa, na ili awajaribu Waumini majaribio mazuri kutoka kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Hayo! Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha njama za makafiri.

Na walipokupangia vitimbi wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe. Na wakapanga vitimbi vyao, naye Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi vyake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wapangao vitimbi.

Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu hali ya kuwa uko miongoni mwao, na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwaadhibu hali ya kuwa wanaomba msamaha.

Kumbukeni pale mlipokuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa kwenye ng'ambo ya mbali, na msafara ulipokuwa chini yenu. Na ingelikuwa mliagana, basi mngelihitilafiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo liliokuwa lazima litendwe. Ili aangamie wa kuangamia kwa ushahidi ulio wazi, na asalimike wa kusalimika kwa ushahidi ulio wazi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Kumbuka Mwenyezi Mungu alipokuonyesha wao katika usingizi wako kwamba wao ni wachache, na lau angelikuonyesha kuwa ni wengi, basi mngeliingiwa na woga, na mngelizozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu akawapa salama. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyo vifuani.

Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyotangulizwa na mikono yenu, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.

Hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuwa ni wa kuibadilisha neema aliyowaneemesha kwayo kaumu, mpaka wao wabadilishe yale yaliyo katika nafsi zao, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Lau lisingelikuwa andiko lililokwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ingewagusa adhabu kubwa kwa vile mlivyochukua.

Basi kuleni katika mlivyoteka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri na kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Ewe Nabii! Waambie wale walio katika mikono yenu miongoni mwa mateka: Kama Mwenyezi Mungu akijua heri yoyote katika nyoyo zenu, atawapa bora kuliko vilivyochukuliwa kutoka kwenu, na atawasitiria dhambi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri na kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Na ikiwa wanataka kukufanyia hiana, basi hakika walikwishamfanyia hiana Mwenyezi Mungu kabla, naye akawawezesha nyinyi kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.