The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Mansions of the stars [Al-Burooj] - Swahili translation - Rowad Translation Center
Surah The Mansions of the stars [Al-Burooj] Ayah 22 Location Maccah Number 85
Ninaapa kwa mbingu yenye nyota kubwa kubwa!
Na kwa siku iliyoahidiwa!
Na kwa shahidi na kinachoshuhudiwa!
Wameangamizwa watu wa makhandaki.
Yenye moto wenye kuni nyingi.
Walipokuwa wamekaa hapo.
Na wao ni mashahidi wa yale waliyokuwa wakiwafanyia Waumini.
Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.
Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu.
Hakika waliowafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.
Hakika walioamini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
Yeye ndiye anayeanzisha na ndiye anayerejesha tena.
Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi.
Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu.
Atendaye ayatakayo.
Je! Zimekuwasilia habari za majeshi?
Ya Firauni na Thamudi?
Lakini waliokufuru wamo katika kukadhibisha.
Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazingira.
Bali hii ni Qur-ani tukufu.
Katika Ubao Uliohifadhiwa.