The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Most High [Al-Ala] - Swahili translation - Rowad Translation Center
Surah The Most High [Al-Ala] Ayah 19 Location Maccah Number 87
Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa.
Aliyeumba, na akaweka sawa.
Na ambaye amekadiria na akaongoa.
Na aliyeotesha malisho.
Kisha akayafanya makavu, meusi.
Tutakusomesha wala hutasahau.
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhahiri na yaliyofichikana.
Na tutakusahilishia yawe mepesi.
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
Atakumbuka mwenye kuogopa.
Na atajitenga mbali nayo mpotovu.
Ambaye atauingia Moto mkubwa.
Tena humo hatakufa wala hawi hai.
Hakika amekwisha fanikiwa aliyejitakasa.
Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
Lakini nyinyi mnahiari maisha ya dunia!
Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo.
Vitabu vya Ibrahimu na Musa.