The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Overwhelming [Al-Ghashiya] - Swahili translation - Rowad Translation Center
Surah The Overwhelming [Al-Ghashiya] Ayah 26 Location Maccah Number 88
Je, imekufikia habari ya msiba wa kufudikiza?
Siku hiyo nyuso zitainama.
Zikifanya kazi, nazo taabani.
Ziingie katika Moto unaowaka.
Zikinyweshwa kutoka chemchemi inayochemka.
Hawatakuwa na chakula isipokuwa kichungu chenye miba.
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
Zitakuwa radhi kwa juhudi yao.
Katika Bustani ya juu.
Hawatasikia humo upuuzi.
Humo imo chemchemi inayomiminika.
Humo vimo viti vilivyonyanyuliwa.
Na bilauri zilizopangwa.
Na matakia safu safu.
Na mazulia yaliyotandikwa.
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyoumbwa?
Na mbingu jinsi ilivyoinuliwa?
Na milima jinsi ilivyothibitishwa?
Na ardhi jinsi ilivyotandazwa?
Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
Wewe si mwenye kuwatawalia.
Lakini anayerudi nyuma na kukataa.
Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!