عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Repentance [At-Taubah] - Swahili translation - Rowad Translation Center

Surah Repentance [At-Taubah] Ayah 129 Location Madanah Number 9

[Huku ni] kujiweka mbali kutokako kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwaendea wale mlioagana nao miongoni mwa washirikina.

Na aondoe hasira ya nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu atamkubalia toba amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwishamnusuru walipomtoa wale waliokufuru, akiwa ni wa pili wa wawili walipokuwa katika pango, alipomwambia sahibu yake: 'Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.' Basi Mwenyezi Mungu akauteremsha utulivu wake juu yake, na akamuunga mkono kwa majeshi ambayo hamkuyaona, na akalifanya neno la wale waliokufuru kuwa chini zaidi, na Neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu zaidi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Lau ingelikuwa ipo faida ya papo kwa hapo, na safari fupi, basi hakika wangelikufuata. Lakini waliona kwamba ni mbali na kuna ugumu. Nao wataapa kwa Mwenyezi Mungu: 'Tungeliweza, basi bila ya shaka tungelitoka pamoja nanyi.' Wanaziangamiza nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika hao ni waongo.

Na wangelitaka kweli kutoka, basi bila ya shaka wangeliliandalia hilo maandalizi ya sawasawa. Lakini Mwenyezi Mungu alichukia kutoka kwao, kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanaokaa!

Lau kama watapata pa kukimbilia au mapango au mahali pa kuingia, basi hakika wangeligeuka kwenda huko huku wanakimbia mbio zisizozuilika.

Wanawaapia kwa Mwenyezi Mungu ili wakuridhishenyi, ilhali Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaostahiki zaidi kwamba wao wawaridhishe ikiwa wao ni Waumini.

Na miongoni mwao kuwa wale waliomuahidi Mwenyezi Mungu kwamba: Akitupa katika fadhila yake, hapana shaka tutatoa sadaka, na tutakuwa katika waliotengenea.

Mabedui ndio wenye ukafiri mkubwa zaidi na unafiki, na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima.

Na katika Mabedui hao kuna yule anayefikiri kuwa kile anachotoa ni gharama ya bure, na anakutazamieni mambo yawageukie. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Na katika Mabedui kuna yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na anakichukulia kile anachotoa kuwa ni cha kumsongeza karibu na Mwenyezi Mungu na cha kupata kwacho dua za Mtume. Ndiyo! Hayo hakika ni mambo ya kuwasongeza karibu. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Je, mwenye kuweka msingi wa mjengo wake juu ya uchaji utokao kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora zaidi au mwenye kuweka msingi wa mjengo wake juu ya ukingo wa shimo unaoporomoka? Kwa hivyo ukaporomoka naye ndani ya Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.

Na mjengo wao huo walioujenga hautaacha kuwa shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Kwa hivyo, wakigeuka, basi wewe sema, ”Mwenyezi Mungu ananitosha. Hakuna mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi ninamtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi."