The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe City [Al-Balad] - Swahili translation - Rowad Translation Center
Surah The City [Al-Balad] Ayah 20 Location Maccah Number 90
Ninaapa kwa Mji huu!
Nawe unaukaa Mji huu.
Na ninaapa kwa mzazi na alichokizaa.
Hakika tumemuumba mtu katika taabu.
Ati anadhani hapana yeyote atakayemuweza?
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anayemwona?
Kwani hatukumpa macho mawili?
Na ulimi, na midomo miwili?
Na tukambainishia zote njia mbili?
Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
Na nini kitakachokujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?
Kumkomboa mtumwa.
Au kumlisha siku ya njaa.
Yatima aliye jamaa.
Au masikini aliye vumbini.
Tena awe miongoni mwa walioamini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.
Lakini waliozikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.
Juu yao utakuwa Moto uliofungiwa kila upande.