The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe night [Al-Lail] - Swahili translation - Rowad Translation Center
Surah The night [Al-Lail] Ayah 21 Location Maccah Number 92
Ninaapa kwa usiku unapofunika!
Na mchana unapodhihiri!
Na kwa aliyeumba dume na jike!
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu.
Na akalisadiki lililo jema.
Tutamrahisishia yawe mepesi.
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake.
Na akakanusha lililo jema.
Tutamrahisishia yawe mazito!
Na mali yake itamfaa nini atakapokuwa anadidimia?
Hakika ni juu yetu kuonyesha uongofu.
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
Basi nakuonyeni kutokana na Moto unaowaka vikali.
Hatauingia ila mwovu kabisa!
Anayekadhibisha na akageuka na kwenda zake.
Na mcha Mungu ataepushwa nao.
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliyemfanyia hisani ndiyo anamlipa.
Ila ni kutaka uso wa Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
Naye atakujaridhia!