The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe morning hours [Ad-Dhuha] - Swahili translation - Rowad Translation Center
Surah The morning hours [Ad-Dhuha] Ayah 11 Location Maccah Number 93
Ninaapa kwa wakati wa kabla ya adhuhuri!
Na kwa usiku unapotanda!
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko uliotangulia.
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
Kwani hakukukuta yatima akakupa makazi?
Na akakukuta umepotea akakuongoa?
Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
Basi yatima usimwonee!
Na anayeomba au kuuliza usimkaripie!
Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie.