The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Fig [At-Tin] - Swahili translation - Rowad Translation Center
Surah The Fig [At-Tin] Ayah 8 Location Maccah Number 95
Ninaapa kwa tini na zaituni!
Na kwa Mlima wa Sinai!
Na kwa mji huu wenye amani!
Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
Lakini wale walioamini na wakatenda mema, hao watapata ujira usiokwisha.
Basi ni kipi baadaye kitakachokukukadhibishia malipo?
Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu zaidi kuliko wote wanaohukumu?